Alice Kimanzi has finally released a video for her jam Waambie. Kimanzi explains that she wrote the song for a friend's wedding which is intended to be a celebration of love as experienced from the bride's perspective. I loved this song the moment I heard it at a Wedding earlier this year. It is now among my favorites and it definitely makes it to my "Banjuka Set" on my big day *Wink*. An expression of simple, honest affection from the heart. *Does My Happy Dance*
Usingizi kanitoroka moyoni nakesha ngoma,
Kwa subira nimengoja penzi hili la thamana,
Tangu tulipokutana nafsi zetu kapatana,
Na ni mbali tumetoka tangu kuchumbiana,
Siku yetu imefika hakuna 'taye zuia,
Ajalie Maulana pete tutavishana,
Waambie mie nimeshapatikana,
Na yule mume wa mapenzi 'sha nienzi,
Waambie mie milele nishazama,
Sinitafute kule kwa mabinti nishahama,
Angalia Ishara {Angalia}
Tazama Ishara {Angalia}
Angalia Ishara {Angalia}
Mi nishahama {Mi nishahama}
Angalia Ishara {Angalia}
Tazama Ishara {Angalia}
Angalia Ishara {Angalia}
Mi nishazama {Mi nishazama}
Kuna wale wanasema ndoa haidumu tena,
Yaje maji na mafuriko tayari tushatia nanga,
Nimempata yule wangu kampenda na vyote vyangu,
Sitajasahau amenivisha dhahabu,
Nimempata yule wangu kampenda na vyote vyangu
Simulia walimwengu nishampa moyo wangu,
Waambie mie nimeshapatikana,
Na yule mume wa mapenzi 'sha nienzi,
Waambie mie nishazama,
Sinitafute kule kwa mabinti nishahama,
Angalia Ishara {Angalia}
Tazama Ishara {Angalia}
Angalia Ishara {Angalia}
Mi nishahama {Mi nishahama}
Angalia Ishara {Angalia}
Tazama Ishara {Angalia}
Angalia Ishara {Angalia}
Mi nishazama {Mi nishazama}
Ee Mola tusaidia kwa wema wako,
Tuwe na ndoa yenye furaha,
Milele hadi milele